Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere amefuta uwezekano wa kusajiliwa tena klabuni hapo, baada ya kusisitiza meneja wa sasa wa The Gunners Mikel Arteta ‘HAMTAKI’.
Kalbu ya kuondoka jumla klabuni hapo msimu wa 2018/19 Wilshere aliitumikia Arsenal katika michezo 200, huku akishinda ubingwa wa Kombe la FA mara mbili.
Akizungumza na Talksport, wakati alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kurudi kwenye kikosi cha Arsenal, Wilshere alijibu: “Meneja hanitaki mimi. Ndio, sidhani kama anataka hilo. Ningependa kurudi Arsenal. Lakini sina uwezo wa kuliwezesha hilo.”
Arteta awali alisisitiza kwamba, kiungo huyo ataendelea kufanya mazoezi na klabu hiyo, lakini hakuna lolote litakalotokea.
Jack Wilshere kwa sasa anafanya mazoezi na kikosi cha Arsenal kilichoweka kambi Falme za Kiarabu ‘UAE’.
“Nafikiri nilikuwa wazi kabisa kuhusu hali ya Jack na nafasi yake; ataendelea kufanya mazoezi tu.” alisema Arteta
Wilshere, ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya kwa kipindi cha mwezi uliopita, lakini hakuna dili lolote lililofanyika.
Klabu ya Lille ya Ufaransa ilihusishwa na mpango wa kumsajili Wilshere, lakini haraka uvumi huo ukafa wakati klabu hiyo ilipothibitisha ujio wa Hatem Ben Arfa.
Jack Wilshere akiwa Arsenal aliwahi kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu za Bolton Wanderers (2010) na AFC Bournemouth (2016–2017), kabla ya uuzwa moja kwa moja West Ham United (2018–2020) kisha akarekejea AFC Bournemouth (2021).