Mshambuliaji wa klabu ya Guangzhou Evergrande ya nchini China, Jackson Martinez, ana ndoto za kutaka kurejea barani Ulaya huku akihusishwa na klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli.

Ndoto za mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia, zimeibuka kutokana na uongozi wa Guangzhou Evergrande kuonyesha upo tayari kumuachia, kutokana na kasi yake ya upachikaji mabao kupunguwa.

Martinez mpaka sasa ameishaifungia klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China mabao mann, tangu aliposajiliwa kwa kiasi cha Euro milion 42, akitokea Altetico Madrid ya Hispania.

Tayari SSC Napoli wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, na kinachosubiriwa ni kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili mwezi januari mwaka 2017.

Real Madrid Wafanya Kweli, Wamuwekea Uzio Vázquez
Chukua Hii: Mpoto ni mtoto wa 36 wa mzee Mrisho