Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameruhusiwa kutoka gerezani na kumalizia kifungo chake akiwa nyumbani kutokana na matatizo ya kiafya.
Idara ya Magereza nchini Afrika Kusini imetangaza msamaha huo ikiwa ni miezi miwili tangu Zuma aanze kutumikia kifungo hicho.
Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kukaidi agizo la Mahakama kuhusu kesi ya rushwa inayomkabili, na alilazwa katika hospitali moja nje ya Mahakama hiyo tangu Agosti 6.
Zuma alifanyiwa upasuaji Agosti 15 mwaka huu ambao hadi sasa haujaelezwa ulikuwa wa nini ila idara ya magereza imesema uamuzi huu mpya umetokana na ripoti ya kiafya waliyoipata kutoka kwa wataalamu wa afya, hata hivyo wamesema wataendelea kumfuatilia ili kuhakikisha anamaliza kifungo chake kwa kufuata masharti aliyopangiwa.