Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo, ameagiza kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Seif for Tobacco Trading Co. Ltd anayefahamika kama Kaissy, aliingiza makontena zaidi ya 500 yenye Molasesi iliyoharibika na kuyatelekeza Bandari ya Dar.

Jafo amesema kuwa Tanzania haiwezi kugeuzwa kuwa dampo kwa kuruhusu bidhaa kutoka nje ya Nchi ambazo muda wake wa matumizi umeisha kuingizwa kwa lengo la kutupwa kiholela.

Aidha, imebainika Mfanyabiashara huyo aliingia nchini kwa hati ya utembezi (tourist) na baadaye kupatiwa kibali cha uwekezaji kupitia Export Processing Zone (EPZA) kilichomruhusu kuwekeza katika uzalishaji wa shisha, kibali ambacho kilifutwa baada ya kugundulika kuna udanganyifu.

Sambamba na hayo, Jafo amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC kufanya ukaguzi katika Bandari kavu zote nchini kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini zikiwa zimeisha muda wake wa matumizi na kutelekezwa.

Bill Gates na mkewe waachana rasmi
Watatu wafariki dunia mgodini