Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa  Mazingira – NEMC, kwa usimamizi mzuri wa sheria ya Mazingira katika mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere – JNHPP.

Pongezi hizo, zimekuja mara baada ya Waziri huyo kuzuru eneo la mradi kwa lengo ili kujiridhisha na hatua za ujenzi zilipofikia sambamba na suala la utunzaji na uhifadhi wa Mazingira katika eneo hilo.

Amesema, “Mradi huu ni mkubwa wenye shughuli kubwa na nyingi zinazozalisha taka za kila aina na idadi ya watu takribani 12,000,  hutegemei kukuta mazingira nadhifu kama haya, hizi zote ni juhudi za  Baraza la Mazingira ambalo lilipiga kambi kabisa hapa kuhakikisha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira inasimamiwa hasa ufanyaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, Hongereni sana.”

Aidha, Jafo amesisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji ya mto kilombero na Ruaha na kuzitaja faida za mradi huu wa kufua umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere kuwa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika, udhibiti wa mafuriko,  uanzishwaji wa kilimo cha maji, kupunguza nishati ya kuni na mkaa na kuongeza ujuzi kwa wataalamu wa Nchi.

Zoezi ukusanyaji Damu lavuka lengo Dodoma
Mzize amepaza sauti ufungaji bora Ligi Kuu