Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, TAMISEMI Sulemani Jafo amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru kutenga angalau Shilingi Milioni 35 ya kufanya matengenezo ya shule ya Msingi Nkuhungu ambayo inabeba wanafunzi wengi.

Jafo ametoa agizo hilo leo Januari 20, 2021 akimtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha anafanya ukarabati wa shule hiyo ndani ya wiki mbili kuhakikisha shule hiyo inafikisha asilimia 100 ya ufaulu kutoka asilimia 91 waliyopo sasa.

Aidha ametoa msisitizo kwa Mkurugenzi na uongozi wa Mkoa huo kukarabati madarasa yote ambayo paa limeharibika kufanyia matengenezo na darasa la awali kufanyiwa maboresho na kuwa la kisasa.

Katika hatua nyingine, Jafo amewaasa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kuhakikisha wanapanda miti ya matunda kwenye barabara zote nchini, kwa lengo la kutunza mazingira na kupendezesha mazingira ya Barabara.

Lampard akalia kuti kavu Chelsea
Mwakalebela: Sarpong hajaachwa Young Africans