Serikali imewaagiza maafisa elimu wote nchini kuboresha mazingira ya shule za msingi na sekondari katika Halmashauri zao wanazoziongoza ili ziwe na mandhari ya kuvutia katika ufundishaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo alipokuwa akitembelea ujenzi wa madarasa, vyoo, na mabweni katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambapo amesema kuwa mazingira mazuri ya kufundishia hutoa hamasa kwa wanafunzi kujitahidi katika masomo.
Aidha, Katika ziara hiyo, Jafo amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi unavyo endelea wilayani humo kwa ulazaji wa matofali katika majengo yote kutokana na ujengaji wa aina hiyo unayafanya majengo kuwa na ubora mkubwa.
Vile vile, Jafo ametembelea na kukagua ujenzi katika Shule ya msingi Kwala ambayo kuna ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu, matundu ya vyoo kumi na mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu.
-
Waziri Lukuvi abanwa, akesha ofisini kwake
-
Vijana waja na mapendekezo maboresho Sera ya taifa
-
Prof. Mbarawa amuweka kitimoto mkandarasi Tabora
Hata hivyo, amewaasa wananchi kujitokeza kushiriki katika ujenzi huo kwani pia kuwahamasisha kuwa waangalifu katika kulinda miundombinu hiyo ambayo itakuwa inatoa huduma kwa wanafunzi alitembelea