Mapema leo hii Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ametembelea katika shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar Es salaam na kutoa maamuzi kadhaa katika shule hiyo kufuatia ufaulu mbovu wa wanafunzi hasa katika matokeo ya mwaka huu ambapo shule hiyo imeshika nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya shule 453 imekuwa ya 451.
Amesema wanafunzi wengi wamefeli kutokana na matumizi ya simu yasiyo ya faida kwao kwani wengi wao hutumia simu hizo kuchat katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook, whatsap pamoja na Instagram ambapo wanajihusisha kuangalia picha zilizokuwa mbovu.
”Kwa taarifa nilizozipata wanafunzi wengine wanatumia simu za watsap wanaangalia picha zilizokuwa mbovu, baadala ya kusoma wanajiandaa kuwa miss Dar es salaam, wengine wanachat na kuangalia picha zisizokuwa safi” Jafo.
-
Jafo atoa siku 1 kufanyika mabadiliko ya uongozi na walimu shule ya Jangwani
-
Nape ajilipua tena, ‘nyekundu iwe nyekundu’
Ameongezea kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanajihusisha na mambo ya uasherati hivyo amewaomba kuachana na tabia hizo ambazo zinawaweka mbali na elimu.
Hivyo amewaonya vikali wanafunzi hao juu ya mambo ambayo hayana faida katika elimu yao na kuwaasa kuacha kujihusisha na mambo yasiyowahusu kwani yanawapotezea muda wa kujisomea.
”Wanafunzi tabia ya kujihusisha na mambo yasiyowahusu kuanzia sasa ishindwe na ilegee”, amesema Jafo.
Aidha amesema changamoto zote zilizotolewa atahakikisha zinafanyiwa kazi ili kuwajengea mazingira mazuri ya kusoma.