Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ametangaza nafasi 3,033 za ajira mpya kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari ambao watakwenda kujaza nafasi za walimu waliotumbuliwa mara baada ya kubainika kutumia vyeti feki.

Jafo amesema kuwa majina ya walimu hao wapya 3,033 yatatangazwa leo na kupangiwa vituo vya kazi, walimu 266 watakuwa ni walimu wa shule za sekondari na Walimu 2,767 watakuwa walimu wa shule ya msingi.

Aidha Jafo amewataka walimu hao wapya ambao wamechaguliwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa halmshauri husika ambazo watakuwa wamepangiwa kuanzia Disemba 27, 2018 hadi Januari 7, 2018.

Mbali na hilo Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu hao wataripoti kuwapokea na kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

 

Rais wa Korea apiga marufuku starehe siku ya krismasi
Meck Sadick aingizwa kamati kuu Yanga