Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewataka viongozi wa Halmashauri nchini kusimamia matumizi ya mapato yanayokusanywa katika Halmashauri zao.
Ameyasema hayo alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Geita na Chato mkoani wa Geita.
Amesema kuwa Halmashauri mbalimbali zinatakiwa kusimamia vyema matumizi ya mapato hayo na kwa kiasi kikubwa yaelekezwe katika miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri.
Aidha, katika ziara hiyo, Jafo amekukagua ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya mji wa Geita, barabara za lami za mji wa Geita zinazojengwa kwa mradi wa ULGSP, zahanati ya Buselesele, Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Chato, pamoja na kutembelea shule ya sekondari ya Magufuli.
-
JUKATA Yataka wabunge watungiwe sheria
-
Mbunge aivimbia TAKUKURU
-
Maafisa Madini wapewa somo utoaji wa leseni
Hata hivyo, Jafo amewahakikishia wananchi wa kata ya Buselesele kwamba serikali itajitahidi ili ijenge kituo cha afya cha kisasa katika kata hiyo ya Buselesele kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo.