Leo Julai 17, 2018 Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amekasirishwa sana na mwenendo wa ufaulu wa shule ya sekondari ya Serikali ya Wasichana iliyopo jijini Dar es salaam, Jangwani, hivyo ameagiza maafisa Elimu Mkoa kwa kusaidiana na Afisa Elimu Wilaya pamoja na Mkurugenzi kufanya mabadiliko ya uongozi pamoja na walimu katika shule hiyo.

”Sijafurahishwa na usimamizi wa shule hii ya Jangwani, Katibu Tawala Mkoa mpaka kesho nataka uwe umefanya mabadiliko ya uongozi katika shule ya Sekondari ya Jangwani, fanya mabadiliko ya uongozi katika shule ya sekondari jangwani, amesisitiza Jafo.

Amemtaka Katibu Tawala Mkoa mpaka kufikia kesho mabadiliko hayo kuwa yamekwishafanyika kwani hajafurahishwi na usimamizi wa shule hiyo.

”Matarajio yangu makubwa ni kuwabadilisha walimu waliokaa zaidi ya miaka mitano hapa na nipate taarifa ofisi kwangu ya mabadiliko hayo”. amesema Jafo.

Aidha amesema katika mabadiliko hayo ahakikishe wale walimu ambao ni tegemeo kubwa kwa shule hiyo wanabakia ila walimu wengine wote waondoke kwani kuna walimu ambao tayari wamefundisha hapo kwa zaidi ya miaka 5 hivyo wanahitaji kubadilisha mazingira ili kuleta walimu wapya na kufanya mabadiliko katika shule hiyo ya Jangwani.

Kufuatia matokea ya kidato cha sita yaliyotoka hivi karibuni, Jangwani imekuwa miongoni mwa shule zilizofanya vibaya na kushika nafasi ya tatu kutoka mwisho, nafasi  ya 451 kati ya shule 453 hali iliyopelekea Jafo kusema Shule hiyo ina unyafuzi wa elimu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Video: Jafo ataja kiini Jangwani kushika mkia matokeo kidato cha sita 2018
Marekani yamnyima VISA Alexis Sánchez