Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa umakini wanao uonyesha katika kusimamia miradi ya barabara hapa nchini.
Ameyasema hayo wilayani Kisarawe alipokuwa akikagua daraja na barabara ya Chole – Tutu – Kihare – Vikumburu ambayo daraja lake pamoja na barabara nzima imejengwa kwa umakini mkubwa.
Barabara hiyo imegharimu shilingi bilioni 1.6 ambayo itakuwa msaada kwa wananchi katika kuimarisha mawasiliano na kukuza uchumi.
Aidha, waziri Jafo amewataka wananchi kulinda miundombinu hiyo ili watu wasipitishe Ng’ombe katika tuta la barabara ili kulinda miundombinu hiyo.
Hata hivyo, sambamba na hilo Jafo amewaagiza TARURA kuweka vivuko vya kuvushia wanyama na kutunga sheria ndogo zataka ili kuepusha uharibifu wa barabara.