Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa agizo kwa halmashauri 12 ambazo ni wadaiwa sugu warejeshe fedha hizo mara moja.

Amesema kuwa hadi kufikia Septemba 30 bodi ilikuwa tayari imetoa mikopo yenye thamani ya Sh9.7 bilioni kwa halmashauri 54 nchini, ambapo amesema kuwa hadi kufikia Septemba 30 fedha zilizorejeshwa ni Sh6.6 bilioni.

Aidha, amezitaja Halmashauri ambazo zimekuwa zkidaiwa kwa muda mrefu kuwa ni pamoja na Mwanza, Mbeya, Moshi, Singida, Kigoma, Karatu, Mbinga, Pangani, Mbinga, Morogoro, Igunga na Kongwa.

“Halmashauri nyingi zimejitahidi kurejesha mikopo kwa wakati lakini kuna zilizoonyesha usugu katika kurejesha mikopo,,” amesema Jafo

Hata hivyo, Jafo ameiagiza bodi kuangalia utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda

 

Video: Sheikh Ponda atakiwa kujisalimisha Polisi
Ni zamu ya waamuzi daraja I na II