Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na uhujumu uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, Elinaza Luvanda amejitoa kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake.
Jaji huyo amejitoa baada ya mshitakiwa namba nne wa kesi hiyo Freeman Mbowe kusema yeye na wenzake hawana imani na jaji huyo na hivyo wanaamini hatowatendea haki.
Mbowe ametoa maelezo hayo baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali mapingamizi matatu yaliyowasilishwa mahakamni hapo na washtakiwa hao.
Mbowe pamoja na mambo mengine amedai kuwa kesi hiyo ina maslahi mapana kwa umma na kulinda maslahi ya Jaji Luvanda.
Wakili wa washtakiwa Peter Kibatala amesema katika hoja zilizotolewa kwenye mapingamizi, hoja ya kwanza Inahitaji vielelezo kutoka Bungeni, hoja ya pili itarekebishwa na hoja ya tatu imekatatliwa.
Kesi hiyo ya Mbowe na wenzake imeahirishwa mpaka pale mahakama itakapopanga Jaji mwingine atakaeendelea kuisikiliza.