Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.JobNdugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwaajili ya matibabu.

Akiwa nyumbani kwa spika Jaji Lubuva pia amemkabidhi Mh.Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi na maaandalizi ya uchaguzi ujao                                    .                                                                                                                               Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara ya SabaSabana na Nanenane katika mpango wa kutoa elimu kwa wananchi.

Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Mh Ndugai ambaye kipindi cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika.

Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kuchangia Pato La Taifa
Ujumbe Huu Umeshika Kasi Mitandaoni