Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amesema kuwa anakerwa na kauli mbali mbali zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa pamoja na wanasheria kuhusu uchaguzi wa Kenya.

Amesema kuwa hakuna chochote cha kujifunza kutoka uchaguzi uliofanyika nchini Kenya kwa mambo yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wao na kutokea kwa dosari kitu ambacho kilisababisha uchaguzi huo kufutwa na mahakama.

Lubuva ambaye alikuwa mwangalizi kutoka jumuiya ya nchi za Madola nchini humo amesema kuwa mambo yaliyofanyika ni yakawaida sana hivyo hakuna cha kujifunza kutoka katika uchaguzi huo.

Amesema kuwa hata maamuzi yaliyotolewa na mahakama  ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi huo yangeweza kutolewa hata hapa nchini endapo Katiba na sheria zingekuwa zinaruhusu.

“Yote hayo ni ya kawaida sana, hatuwezi kusema Kenya ni mfano wa kuigwa katika kile kilichotokea, wamefanya hivyo kulingana na mazingira yao kwakuwa yanawaruhusu kufanya hivyo,”amesema Jaji Lubuva.

Hata hivyo, Jaji Lubuva amesema kuwa amekuwa akikerwa na baadhi ya wanasiasa na wanasheria kwa kauli yao ya kusema kuwa majaji au watendaji wa tume hawako huru, kitu ambacho amekipinga vikali.

Manchester City yaichapa Liverpool
Video: Madereva wengi wanadharau- Kamanda Msangi