Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hakutakuwa na mwanya wa kuiba kura katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa tume hiyo imepiga marufuku usafirishaji wa mabox ya kura baada ya zoezi la kupiga kura.

Jaji Lubuva ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa walemavu kuhusu namna bora ya kuboresha ushiriki wa walemavu katika upigaji kura.

“Kura zote za urais, ubunge na udiwani zitahesabiwa na matokeo yatabandikwa katika kila kituo, wanaposema kura zitaibiwa zitaibiwaje,” alisema Jaji Lubuva.

Alifafanua kuwa matokeo ya kura za udiwani yatapelekwa katani kwa ajili ya kujumlishwa na mshindi atatangazwa hapo. Pia, kwa matokeo ya ubunge yatapelekwa jimboni ambapo mshindi atatangazwa hapo pia huku matokeo ya urais yakitumwa NEC kwa njia ya mtandao baa ya fomu za matokeo kuskaniwa.

Pellegrini Angewashuhudia Man City Kideoni
Ian Wright Amshangaa Arsene Wenger