Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Benhajj Shaaban Masoud amewataka wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufaa kutumia vyema elimu ya uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye Sekta ya Sheria na Haki.
Wakati akifunga Mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Masoud amewaeleza washiriki kwamba, wananchi wanaamini mahakamani ni mahali pa kupata haki.
Masoud amewataka maafisa wa Mahakama kutambua umuhimu walionao kwa wananchi wanaowahudumia na kuwaomba maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo.