Jaji Mkuu wa Tanzania Pro. Ibrahim Hamis amezita taasisi mbalimbali zinazosimamia utekelezaji wa sheria na haki za binadamu kuongeza ufanisi wa kutoa huduma hasa maeneo ya vijijini.

Ametoa maelekezo hayo kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA).

Jaji Mkuu Prof. Ibrahim amesema kuwa upatikanaji wa huduma za kisheria maeneo y vijijini bado ni mdogo ambapo amesema watu wanaoishi maeneo hayo wanahitaji utatuzi wa kisheria kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo ya Urithi na matatizo ya kifamialia

Naye mwenyekiti wa TAWLA nchi Lulu Mwanakilala pamoja na kueleza mafanikio ya kutetea haki za wanawake na watoto, katika kipindi cha miaka 30, amesema jamii bado inahitaji kupatiwa elimu ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia.

Museveni atangaza kupata dawa ya virusi vya corona
Sven: Hatujamaliza kazi