Jaji Joachim Tiganga amejitambulisha katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya washtakiwa na upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena leo Jumanne Oktoba 26, 2021 baada ya kusimama kwa siku saba, tangu Oktoba 20, huku Jaji Kiongozi Mustapha Siyani aliyekuwa akiisikiliza alipojitoa kutokana na kuongezewa majukumu.
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Ruswa na Uhujumu Uchumi inayosikiliza kesi hiyo ilitoa hati ya wito kwa pande zote katika kesi hiyo kufika mahakamani leo kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.
Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi