Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amevikumbusha vyama kutii sheria ya gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchauzi.
Ametoa wito huo kupitia barua aliyoiandika kwa vyama ya kutaka kuvikumbusha vyama hivyo kuzingatia sheria na kanuni za sheria ya gharama ya uchaguzi.
“Natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zinazoendelea, katika Majimbo na Kata, hivyo naviasa vyama vya siasa kuheshimu na kufuata sheria za nchi, hasa sheria ya vyama vya siasa, sheria ya gharama za uchaguzi na kanuni zake kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi,”amesema Jaji Mutungi katika barua hiyo.
Hata hivyo, Jaji Mutungi ametoa wito kwa chama chochote cha siasa kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko kujichukulia sheria mikononi, endapo kitaona sheria za uchaguzi zinazofanyika zinavunjwa.
-
Kigwangalla: Najitoa kupigania maliasili zetu natukanwa na kushambuliwa
-
Serikali Yakataa Kuvunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
-
Watu 7 watiwa mbaroni wizi wa pikipiki