Msajili wa vyama vya siasa  Jaji Francis Mutungi amewataka waandishi wa habari kusaidia kuwaondoa hofu wananchi kuhusu hofu na taharuki inayoendelea kujengeka kuhusu uvunjifu wa amani pasipo msingi katika mandamano yanayotarajiwa kufanywa baadhi ya vyama vya siasa Agosti 31 na septemba mosi mwaka huu.
Hayo  yamesemwa leo na msajili wa vyama vya siasa nchini jaji Francis Mutungi  jijini Dar es salaam,alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa wananchi wasiamini kuwa kuna ombwe la kiutendaji na kubaki njiapanda kwamba hakuna njia ya kufikia suluhu au kupata muafaka katika mambo yanayo endelea katika duru za siasa hapa nchini.
Aidha amewaomba wadau wote na vyama vya siasa wanaoitisha maandamano kuwa na subira na kufanya mazungumzo kwa kuwa anaamini katika mazungumzo muafaka utapatikana,na utawala bora ni pamoja na kuheshimu taratibu zilizopo.
Pamoja na hayo Mutungi amesema baraza la siasa litafanya vikao mfululizo tarehe 29 na 30Â mwezi huu na kikao hicho kitakuwa maalumu kwa mazungumzo kwaajiri ya kutafuta kufikia suluhu ya jambo hilo la maandamano.