Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa kusimamisha makongamano na mikutano mbalimbali, ili kupisha mazungumzo kati ya wadau wa siasa.

Mutungi amesema hayo leo Septemba 6 jijini Daar es Salaam akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili kwa pamoja na kujenga taswira nzuri ya nchi kwa kuwa Tanzania sio nchi inayoongozwa na jeshi

Amesema kwamba mkutano huo utahusisha viongozi wa kisiasa, Jeshi la Polisi na Ofisa ya msajili wa vyama na mikutano itaendelea pale mazungumzo yatakapomalizika na kufikia muafaka wa namna nzuri kufanya mikutano bila kuhusisha polisi.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa siku za hivi karibuni majibizano yameibuka kwenye mitandao juu ya maswala ya uhuru wa vyama vya siasa na serikali haina lengo la kuvunja katiba bali kutaka kusimamia kila chama kifanye makongamano kwa kufuata taratibu za nchi na kusimamia amani.

Mkutano huo wa wadau wa Siasa unakuja baada ya siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vya siasa kuzuiliwa kufanya makongamano ya kisiasa na kulishutumu jeshi la polisi kutojali uzalendo wa wananchi.

Jaji ajitoa kesi ya Mbowe
Jacob Zuma aondolewa gerezani