Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amejiondoa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mwenzake watatu.

Jaji Siyani amejitoka kuendesha kesi hiyo leo Oktoba 20, 2021, kwa kile alichodai kuwa kwa sababu ya uwingi wa majukumu unaotokana na uteuzi alioupata hivi karibuni.

Amesema uwingi wa majukumu aliyonayo yanaweza kumfanya ashindwe kuendesha kesi hiyo kwa haraka.

Jaji Siyani ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu HAssan na kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ametangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya kutoa maamuzi ya kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Mbowe na kutupilia mbali mapingamizi ya Mbowe.

Azam FC kuifuata Pyramids FC leo
Mahakama yatupilia mbali pingamizi la mbowe na wenzake