Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba amesema Serikali haina uwezo wa kuajiri wahitimu wote hivyo vyuo vitumie mbinu za ziada kuwajengea uwezo wa kujiajiri wanafunzi pindi wanapohitimu.

Jaji Warioba amesema Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinawajengea wanafunzi msingi wa kujiajiri kwa elimu wanayotoa hivyo ametoa rai kwa vyuo vingine kutumia mbinu hiyo ili changamoto ya ajira ipungue.

Akizungumza katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Kitaifa ya Hayati Edward Moringe Sokoine uliofanyika Viwanja vya SUA Morogoro, Jaji Warioba amesema Watanzania walio wengi bado ni masikini.

Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema tangu Uhuru, Tanzania imepiga hatua kubwa mpaka kuingia Uchumi wa Kati lakini bado yapo matatizo hasa katika eneo la umasikini.

Aidha, amesema Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango wamefanya Watanzania waamini Taifa lipo salama.

Mwenye timu yake amerudi
Wawili wakamatwa kwa mauaji