Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Sinde Warioba amewataka wanasiasa kujenga utamaduni wa kuwa wanakutana pindi wanapoona kuna matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Jaji Warioba amesema kuwa waasisi wa Taifa walijenga umoja na misingi ya maendeleo ambayo kuna kila dalili ya kutoweka kulingana hali ya mambo inavyokwenda inabadilika badilka.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua mdahalo wa mashauriano juu ya kuhamasisha, kusisitiza, kulinda na kudumisha amani na maridhiano nchini ambayo ndio msingi mkuu wa mshikamano.

Amesema kuwa kuna viashiria vya kutoweka kwa amani na viongozi wa kiserikali na kisiasa wanapaswa kuiga kile kinachofanywa na viongozi wa dini ambao wamekuwa na kawaida ya kukutana mara kwa mara.

“Amani ikitoweka kuirudisha ni shida au kuiendeleza, viongozi hasa hawa wa kisiasa wanapaswa kuwa wepesi kukutana na kuzungumza, tuache malumbano hasa tukiwafuata hawa wanasiasa wanaweza kutufikisha pabaya,”amesema Jaji Warioba

Hata hivyo, Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kukaa pamoja na kutafuta namna ya kutatua matatizo mbalimbali ili kuweza kufikia muafaka ambao utaendelea kudumisha amani na mshikamo.

Claude Puel ataeuliwa kuwa kocha mpya Leicester City
Lulu akutwa na hatia ya kuua bila kukusudia, hukumu yake kutolewa Novemba 13