Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa FIFA Juma Ally Khamis kilichotokea jana kisiwani Pemba.

Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu na kusema TFF ipo pamoja na wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Wakati wa uhai wake marehemu Juma Ally Khamis alikuwa mwamuzi mwenye beji ya FIFA, mkufunzi wa waamuzi Tanzania, Meneja wa uwanja wa Amani – uliopo Zanzibar na mratibu wa michezo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Alhamis nyumbani kwake Pemba.

Man Utd Wafikiria Kumrejesha Nyumbani Adnan Januzaj
Mpango wa Kupakua Kamati Za Bunge Huu Hapa