Kiungo wa Simba, James Agyekum Kotei amejiunga na klabu ya soka ya Kaizer Chiefs  ya nchini Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kaizer Chiefs ambayo ilimaliza katika nafasi ya 9 msimu uliopita, imethibitisha kumsajili nyota huyo raia wa Ghana ambaye alifanya vizuri akiwa na klabu ya Simba msimu uliopita.

Kotei alisajiliwa na Simba Disemba 2016, muda mfupi baada ya kufanya majaribio ya kujiunga na kikosi cha Simba na kufuzu.

Aidha, mchezaji huyo aliisaidia Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ilipofika robo fainali na alichaguliwa kuwa kiungo bora kwenye tuzo za Mo’ Simba Awards.

Hata hivyo, mpaka sasa haijawekwa wazi ni kiasi gani Simba wamevuna kwenye usajili huo kutokana na kumuuza Kotei ambaye alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 27, 2019
Iran yaitaka Marekani kutii makubaliano ya mwaka 2015

Comments

comments