Beki wa klabu ya Burnley James Tarkowski ameondolewa katika orodha ya kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu ya taifa ya England, kilichoingia kambini kujiandaa na fainali za kombe la dunia, zitakazoanza Juni 14 nchini Urusi.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 28, alianza kuitumikia timu ya taifa ya mwezi March wakati a michezo ya kimataifa ya kirafiki, na alitajwa kwenye orodha ya watu watano wanaounda kikosi cha akiba cha kocha Gareth Southgate, ambao wamejumuishwa kwenye mazoezi ya The Three Lion yanayoendelea St George’s Park.
Tarkowski akiwa katika kambi ya timu hiyo, alipatwa na majeraha ya nyonga, ambayo kimahesabu yanampa nafasi finyu ya kucheza fainali za kombe la dunia, endapo angeteuliwa katika kikosi cha mwisho cha England kitakachokwenda nchini Urusi.
Beki huyo pia ana tatizo la Mshipa (Hernia), ambalo linamlazimu kufanyiwa upasuaji mdogo katika kipindi hiki, hivyo benchi la ufundi la timu ya taifa ya England limeona kuna haja ya kumuweka pembeni.
Kufuatia maradhi hayo, Tarkowski huenda akawa fit, wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi (2018/19) ambao rasmi unatarajia kuanza mwezi Julai.
Hata hivyo bado kocha mkuu Gareth Southgate, hajatangaza maamuzi ya kumteua mchezaji mwingine ambaye atachukua nafasi ya Tarkowski ama kuacha wazi nafasi hiyo.
Wachezaji ambao huenda wakatajwa kujaza nafasi hiyo, kufuatia mwenendo wa hali zao na uwezo waliouonyesha siku za karibuni ni Tom Heaton, Lewis Cook, Jake Livermore na Adam Lallana.
-
Video: Jinsi Bale alivyosherekea ushindi na mashabiki Madrid
-
Video: Madrid yaweka historia UEFA Champions League
Kocha Southgate bado ana muda wa kufanya maamuzi hadi Juni 04, ambapo atatangaza kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23, ambacho kitakwenda kushiriki fainali za kombe la duinia nchini Urusi.