Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England Leicester City, Jamie Vardy hii leo anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya huko kaskazini mwa jijini London ikiwa ni sehemu ya uhamisho wake wa kujiunga na Arsenal.

Mpango wa uhamisho wa mshambuliaji huyo, ambaye msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 24 katika ligi ya nchini England, ulianza mwishoni mwa juma lililopita kwa Arsenal kuwasilisha ofa ya Pauni milioni 20 huko King Power Stadium.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti la The Sun zinaeleza kwamba, mazungumzo baina ya uongozi wa Leicester City na ule wa Arsenal yamekwenda vyema, na hii leo Verdy huenda akaruhusiwa kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya England ili kukamilisha mpango wa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya yake.

Tukio la kupimwa afya kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 limepangwa kufanyika London Colney.

Cristiano Ronaldo Apigania Hatma Ya James Rodriguez
Philippe Coutinho Azigonganisha FC Barcelona, Paris Saint-Germain