Kadala Komba – Chemba.

Mratibu wa Miradi Women Wake Up – WOWAP, Nasra Suleimani  ameiasa jamii kuhakikisha wanasaidia kutimiza ndoto za watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kutokomeza mimba za utotoni na vikwazo vyote ambavyo vinamkuta mtoto wa kike katika kukwamisha ndoto zake za kufikia kielimu.

Nasra ameyasema hayo Wilayani Chemba katika Kijiji cha Kwamtoro kilichopo Kata ya Kwamtoro kwenye mkutano wa nje na  Wazazi wa kijiji hicho, uliolenga kuhamasishaji jamii pamoja na kuwapatia Elimu namna bora ya kuwasaidia watoto wa kike kutimiza ndoto zao kuanzia  ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Amesema, “tumekuwa tukiufanya mradi huu kwa nguvu kubwa katika mashule lakini kutoka na ambavyo tumekuwa tukipata mrejesho  kutoka kwa wanafunzi  namna ambavyo wazazi wamekuwa hawana ukaribu na watoto wao, hivyo tukasema tunahaja ya kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kuwafikia wazazi.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa Women Wake Up, Luhaga Makunja amesema dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha wazazi  kutatua vikwazo vinavyosababisha watoto wadogo hasa wasichana kukatiza masomo yao, hasa wale waliokatisha masomo kutokana na ujauzito wakati sheria inawaruhusu.

“Kumekuwa na dhana mbaya kwa jamii na mtazamo hasi kwamba mwanafunzi ambaye alishapata mimba  anaporudi shuleni wenzao kuwazomea na kukosa mahitaji muhimu na kuweza kuboresha mazingira ya shuleni, ili waendelee na masomo na kutimiza ndoto zao,” alisema Makunja.

Naye Afisa Mtendaji Kata ya Kwamtoro, Evaresto Mahenge na Mzazi Mwasiti Issa kwa nyakati tofauti wameishukuru timu ya Women Wake Up kwa mafunzo waliyofanya  kwenye kata yake, akiamini yatawasaidia watoto wa kike kufikia ndoto zao kielimu,elimu hasa ambao waliacha shule kwa muda kutokana na changamoto mbalimbali ambao watafutiliwa na kurudishwa mashuleni.

Vilevile, Tizo Wambura mkazi wa Kijiji cha Kwamtoro ambaye pia ni Mwanakamati wa Shule ya Msingi Kwamtoro amelishukuru shirika hilo kwa kutoa semina Shuleni lakini pia mahali popote ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa watu katika viahatarishi ambapo wakipata elimu itawasaidia kuijenga jamii iliyo bora.

Miquisson ajibebesha jukumu Simba SC
Lukaku amuibuka Rais Inter Milan