Ugonjwa wa Saratani, umeongezeka kwa kasi Mwaka 2020 ambapo unaonesha vifo vipya zaidi ya Elfu 40 na vifo Elfu 26,945 ikiongozwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi, tusipochukua tahadhari ugonjwa wa Saratani unaweza kufikia vifo Mil. Moja ifikapo Mwaka 2050.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati akizindua kampeni ya kuelimisha jamii juu ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika katika Hospitali ya Sinza iliyopo eneo la Palestina Jijini Dar es Salaam.

Amesema, “takwimu zinaonesha magonjwa hayo yameongezeka kwa mara Tano hadi Tisa zaidi kati ya miaka ya 80 ambapo asilimia Moja tu ya Watanzania walikua na tatizo la Kisukari na 5% walikua na tatizo la Shinikizo la juu la Damu na sasa Kisukari 9% na Shinikizo la Damu 25%.”

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Saratani yanachangia kwa asilimia 33 ya vifo vyote nchini Tanzania na kwamba jamii inapaswa kuwa makini na mtindo wa maisha ikiwemo kuachana na ulaji wa vyakula bila mpangilio na kupunguza matumizi ya unywaji wa Pombe.

Ukarabati wa uwanja wa Mkapa kuwahi ufunguzi AFL
Watanzania waaswa kupunguza matumizi ya Pombe