Mshambuliaji wa pembeni Adnan Januzaj amepelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Borussia Dortmund akitokea Old Trfford yalipo makao makuu ya klabu ya Man Utd huko nchini England.

Dili la kuuzwa kwa mkopo la Januzaj lilikamilika usiku wa kuamkia hii leo baada ya uongozi wa Borussia Dortmund kukubali masharti kadhaa likiwemo suala la ada ya uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji huyo.

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amesema kusajiliwa kwa Januzaj kutawasaidia mno kwenye kikosi chao ambacho kilionyesha kuhitaji huduma ya mshambuliaji kama kinda huyo kutoka nchini ubelgiji.

Zorc amesisitiza kuona amambo mazuri yakimnyookea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20, kwa kusaidiana na wachezaji wengine klabuni hapo kwa ajili ya kusaka mafanikio msimu huu wa 2015-16.

Kwa upande wake Januzaj amesema hana sababu ya kujutia maamuzi ya kujiunga na klabu ya Borussia Dortmund, zaidi ya kufurahia dili hilo kukamilishwa ipasavyo, kutokana na ukubwa na umuhimu wa klabu hiyo ambayo imekua ikionyesha hitaji la kusaka mafanikio duniani kote.

Januzaj, alijiunga na Man Utd mwaka 2011, akitokea nchini Kwao Ubelgiji alipokua akiitumikia klabu ya Anderlecht, na mpaka anaondoka Old Trafford usiku wa kuamkia hii leo, alikua amefanikiwa kuiwatumikia mashetani wekundu katika michezo 45 na kufunga mabao matano.

Man Utd Wampata Mbadala Wa Wayne Rooney
De Gea Mashakani Kurejea Nyumbani