Mradi wa kutengeneza gari lenye uwezo wa kupaa umeanza rasmi nchini Japan.
Kulingana na vyombo vya habari vya Japan kampuni 20 zinashirikiana katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Uber, Japan Airlines, Airbus, Boeing, NEC, Toyota, ANA na Yamato ni kati ka kampuni zinazohusika na utengenezaji wa gari hilo la kipekee.
Wizara ya uchumi, biashara na viwanda nchini Japan imesema kuwa mradi huo utatumia bajeti ya $ 40.4 milioni.
Na gari hilo la kupaa bila ya dereva linatarajia kukamilika ifikapo 2020 na kuzinduliwa katika sherehe za mashindano ya Olympic 2020 huko Tokyo.
Aidha gari hiyo litakuwa moja kati ya magari ya gharama zaidi duniani, kutokana na upekee wake lakini pia gari hiyo itatatua changamoto ya foleni hasa kwenye zile nchi zenye msongamano wa magari kama ilivyo hapa Dar es salaam ambako kuna tatizo kubwa la miundombinu ya barabara kuwa michache na mibovu inayopelekea uwepo wa foleni kubwa hasa kipindi cha mvua.