Kumekuwa na matumaini makubwa kwamba dawa ya remdesivir ingeweza kutibu ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, lakini imeripotiwa kushindwa kufikia viwango vya ufanisi katika jaribio la kwanza la matibabu.

kwa mujibu wa waraka uliochapishwa kimakosa na Shirika la Afya Duniani (WHO), jaribio la dawa hiyo nchini Uchina limeonesha kuwa haikufanikiwa,

Waraka huo umesema Dawa hiyo haikuboresha hali za wagonjwa au kupunguza kiwango cha virusi katika damu.

WHO imethibitisha kuwa ripoti hiyo ya muswada iliwekwa mtandaoni kimakosa ambayo inaonesha kuwa watafiti waliwafanyia uchunguzi wagonjwa 137, wakawapatia dawa 158 na kulinganisha mafanikio na waliosalia 79, ambao walipewa dawa isiyo na kemikali ya placebo.

Kampuni ya Marekani inayotengeneza dawa hiyo, Gilead Sciences, imesema kuwa waraka huo ulipotosha uchunguzi wake.

“Tunaamini kuwa taarifa iliyotumwa ilijumuisha data zisizofaa kuhusu utafiti,” msemaji wa kampuni ya Gilead alisema na kuongeza kuwa utafiti ulisitishwa mapema kutokana na kujitokeza kwa watu wachache kushiriki na hivyo takwimu zake hazikuwa na maana.

EU yaonya matumizi ya dawa za Malaria kutibu Corona
Bei elekezi ya sukari nchini 2,600/= hadi 3,200/=