Mapigano ambayo yaliukumba mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown yanadaiwa kusababisha vifo vya wanajeshi 13 wa jeshi tiifu kwa Serikali, ambapo yalikuwa yamepangwa na Wanajeshi walioko kazini na waliostaafu.

Msemaji wa Jeshi, Kanali Issa Bangura amesema wameondoa amri ya kutotoka nje wakati wa mchana ambayo ilikuwa imewekwa na kuwataka watu warejee tena katika maisha yao ya kila siku, huku wakitakiwa kuendelea kuwa makini.

Amesema, “tumeanzisha msako wa kuwakamata wote waliohusika katika shambulio hilo la kikatili, miongoni mwao wakiwa wanajeshi waliopo kazini na wastaafu. Baadhi ya maduka na benki zilifunguliwa na usafiri wa magari ulianza tena.”

Sierra Leone ni nchi ya Afrika Magharibi inayozungumza Kiingereza, ambayo imekuwa ikipitia mzozo wa kisiasa kufuatia uchaguzi wa mwezi Juni na tayari vituo vya ukaguzi vimewekwa kwenye barabara kuu, kwa ajili ya upekuzi.

Wakati huohuo, watu wamekuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusiana na kilichotokea nchini humo, huku kukiwa na hofu ya kutokea mapinduzi mengine katika eneo hilo la Afrika Magharibi, kwa Nchi za Mali, Burkina Faso, Niger na Guinea zote zimekumbwa na misukosuko tangu 2020.

Ahmed Ally afichua ujio wa Benchikha
Nunez kuichomoa pesa Liverpool