Promota mashuhuri wa masumbwi nchini, Jay Msangi ametangaza nia ya kuwania kiti cha Urais wa kamisheni ya kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) katika uchaguzi mdogo wa kamisheni hiyo unaotarajiwa kufanyika Mei 08 mwaka huu 2022.
Nafasi ya urais wa TPBRC imekuwa ikikaimiwa na Agapeter Basili ambaye alikuwa Makamu Rais, tangu kujiuzulu kwa Joe Anea ambaye alichukua hatua hiyo ya kujiuzulu kutokana na changamoto za kiafya.
Akizungumzia sababu za kutangaza hadharani kuwania kiti cha Urais wa TPBRC Msangi amesema: “Nimejipima nimeona natosha, naamini nitakuwa great asset kwa shirikisho la ngumi za kulipwa, Nina experience ya kutosha katika uongozi, ninaufahamu mchezo wa ngumi za kulipwa kindaki ndaki na pia ninayafahamu matatizo, changamoto za mchezo wa ngumi wanazozipata wadau wake kwa ujumla”
“Nawaahidi wadau wangu nitakuwa mwaminifu, msikilizaji mzuri na mtekelezaji, nina utaalamu wa kutatua changamoto, Problem solving Skills, INOVATION ( uvumbuzi ) CREATIVE (ubunifu).”