Rapa kutoka Marekani JAY-Z ameonekana kuthibitisha kuwa mama yake ni mpenzi wa jinsia moja, katika wimbo uliopo kwenye albamu ya 4:44 JAY-Z kuna mistari inayosema;Mama alikuwa na watoto wanne lakini ni mpenzi wa jinsia moja licha ya kujifanya kuwa muigizaji.
Katika wimbo huo imesikika sauti ya mama yake JAY-Z kwenye (autro) maneno ya mwishi wa wimbo akisema ”Dunia inabadilika na wanasema ni wakati wa kuwa huru/lakini unaishi na hofu ya kuwa wewe mwenyewe”
”Kuishi katika kivuli kunaonekana kuwa eneo salama kuwa, hakuna mtu wa kukushambulia /lakini maisha ni mafupi na ni wakati wa kuwa huru”.
-
Future Amjibu Jay Z, ni Baada ya Mstari wa Jigga Kudaiwa ‘Kumchapa’
-
Picha: Ronaldo aionesha dunia anachojivunia
JAY-Z ambaye albamu yake ya 4:44 amekuwa miongoni mwa albamu zinazofanya vizuri sokononi kwa sasa hajawahi kuweka wazi kuhusu mama yakeGloria Carter juu ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja katika nyimbo zake.