Kampuni maarufu ya vinywaji ya Coca-Cola inapanga kufanya majaribio ya aina mpya ya kinywaji ambacho kitatokana na Bangi

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa BNN Bloomberg, kampuni hiyo itashirikiana na kampuni mwenyeji ya kutengeneza bangi kwa jina Aurora Cannabis.

Aidha, lengo kuu la kuwa na kinywaji hicho litakuwa ni kupunguza uchovu na si kuwalewesha watu ambao watakuwa wanatumia pombe hiyo.

“Kwa pamoja na wadau wengine wengi katika sekta hii ya vinywaji, tunafuatilia kwa karibu ukuaji wa soko la vinywaji vyenye bangi aina ya cannabidiol visivyolewesha kama kiungo katika vinywaji vya kuboresha afya maeneo mengi duniani,” imesema taarifa kutoka Kampuni ya Coca-Cola.

Hatua ya Coca-Cola imejiri huku Canada ikijiandaa kufanya mazungumzo na majimbo ya Marekani ambayo hivi karibuni yameidhinisha matumizi ya bangi kwa sababu za kujiburudisha, baada ya kukubali matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu kwa miaka mingi.

Douglas Costa atupwa jela, kukosa michezo minne
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 19, 2018