Suala la usajli wa laini kwa alama za vidole kwa kutumia namba ya utambulisho ya kitambulisho cha Taifa cha NIDA limekua na kuzua gumzo kwa watanzania wengi ambao bado hawajafanikiwa kusajili laini zao kufuatia sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
Wengi wameonesha kukata tamaa na kususia zoezi hilo kufuatia usumbufu unaojitokeza hasa katika zoezi la upatikanaji wa kitambulisho cha taifa ambalo linagharimu muda wa kutosha hasa katika kukusanya viambatanisho muhimu vitavyomtambulisha mtu na utaifa wake.
”Ishu ni kwamba watu wamejiandikisha ila suala la kupata namba au kitambulisho ndiyo imekuwa mchakato, Fungeni tuuu hizo laini tule hasara wote”
”Fungeni msitusumbue makampuni yenu yapate hasara wafanyakazi wapunkuzwe kodi zipungue”
Baadhi ya maoni ya watu mara baada ya Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba kutoa angalizo kufutia siku chache zilizobaki kufungwa kwa laini hizo huku akisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.
Aidha, wengi wametupa lawama kwa NIDA, kukwamisha zoezi la uasjili wa laini izo kwa madai kuwa wengi wamemaliza taratibu zote za usajili wa vitambulisho vya taifa lakini bado hawajapa namba wala kitambulisho jambo ambalo linakwamisha usajili wa laini zao kwa alama za vidole.
”Kumfungia laini mtu ni sawa na kuharibu mipango yake, mi naona kuna watu wanashabikia hili suala wangekua wanajua ugumu tunaoupata kupanga foleni kuanzia alfajiri hadi jioni utasikia mtandao unasumbua tunaacha kufanya kazi za kimaendeleo na tulijisajili kitambo, halafu TCRA inaangalia upande mmoja. Fungeni ila Mungu anawaona!!!!!!” ameandika mkereketwa wa zoezi hili la usajili Bwana Solmon Edward Zakaria.
”Jamani wengine tutaonewa bure NIDA hawajatoa namba sasa tutafanyaje ikiwa ukienda NIDA unaambiwa baada ya wiki tatu ukirudi unaambiwa hivyo hivyo yaani nashindwa kuelewa kabla TCRA hamjafunga laini zetu Kwanza nendeni nida muwaulize je mmetoa namba za NIDA kwa walengwa wote? ndo mje mfanye maamuzi” maoni ya mtanzania mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.
Aidha suala la usajili wa laini kwa alama za vidole kila mtu analichukulia kwa mtazamo tofauti, ni dhahiri endapo bado idadi kubwa ya watanzania watafungiwa laini, kutatokea sintofahamu kubwa sana hasa upande wa mawasiliano hasa kwa vijijini ambapo bado wapo nyuma hasa katika upatikanaji wa taarifa muhimu kama hizi.
Hata hivyo mara ya kwanza zoezi hili lilitamkwa kusitishwa Disemba 31, 2019, hadi pale baadaye Rais Dk. John Pombe Magufuli alipotamka kuongezwa kwa siku 20 kwa zoezi hilo lakini bado idadi kubwa ya watanzania wameshindwa kutumia siku hizo kukamilisha usajili.
Pia wapo zaidi ya watanzania milioni 6 kwa mujibu wa NIDA wanavitambulisho/namba za utambulisho wa taifa lakini bado hawajasali laini zao kwa alama za vidole, Changamoto juu ya changamoto.