Mshambuliaji wa Simba SC Jean Othos Balake
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi
wa mwaka 2022/23, huku Kocha Mkuu wa
akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.
Kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 8, 2023, kimemchagua Baleke, baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Machi na kutoa mchango mkubwa kwa Simba, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu katika dakika 81 alizocheza, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini.
Baleke amewashinda Daruweshi Saliboko wa KMC na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons alioingia nao hatua ya fainali. Kwa mwezi Machi kila timu
ilicheza mchezo mmoja tu.
Kwa upande wa Oliveira aliwashinda Nasreddine Nabi wa Yanga na Abdallah Mohammed wa Tanzania Prisons katika hatua ya fainali, ambapo kwa mwezi huo Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Highland Estates Mbarali, Omary Malule kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi, kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.