Aliyewahi kuwa kiongozi wa Waasi, Jean Pierre Bemba amekataliwa kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Tume ya Uchaguzi imemuondoa Pierre Bemba kwenye kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na wagombea 6, ambapo kwasasa anaungana na Moise Katumbi ambaye pia alipigwa marufuku kuingia nchini humo.

Aidha, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, imesema kuwa Bemba ameondolewa kwa tuhuma za kuwahonga mashahidi katika kesi yake ya uhalifu wa kivita huko ICC.

Hata hivyo, Bemba alikutwa na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita na Mahakama ya ICC mwaka 2016 lakini aliachiwa huru baada ya kushinda rufani yake Julai mwaka huu.

Madeni yamvuruga Msemaji wa Serikali
Video: Mjumbe wa CCM mkoa wa Simiyu afunguka hamahama ya Wapinzani