Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha jana alihitimisha zoezi la uchaguzi wa marudio kwa kumtangaza Dk. Ali Mohammed Shein (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha urais huku akiutaja Uchaguzi Mkuu unaofuata.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyosomwa na Jecha, Dk. Shein alishinda kwa kishindo cha asilimia 91.4, ushindi ambao haujawahi kuripotiwa katika historia ya chaguzi za Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Akizungumza katika hotuba yake fupi, Mwenyekiti huyo wa ZEC aliwataka waliokuwa wagombea wa vyama vingine vya siasa walioshindwa katika uchaguzi huo kusubiri tena mwaka 2020, akituma maneno ‘tutaonana 2020’.

Baada ya hotuba yake, Jecha hakuonekana nje ya ukumbi na aliondoka bila kuonekana kama alivyoingia.

Habari Mpasuko: Chadema yashinda 'Umeya' wa Dar
BBC: Guardiola Hawezi Kuchomoka Man City