Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi Mkoani Morogoro, imemhukumu kifungo cha maisha jela Ezekiel Christopher Kidula kwa kosa la kukutwa na bangi nyumbani kwake yenye uzito wa kilo 198.41 kuagiza kuteketezwa kwa bangi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo Aprili 28, 2023 Jaji Mstapha Ismail alisema, ushahidi wa upande wa Jamhuri umethibitisha pasipo shaka yoyote kwamba, mtuhumiwa alitenda kosa hilo. Hivyo, Mahakama ilimtia hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya.

Alisema, ‘‘utetezi uliotolewa na Wakili wa mshtakiwa kuwa mshtakiwa hajawahi kutenda kosa la jinai na ana umri mkubwa ila kutokana na ukubwa wa kosa lililomtia hatiani na madhara ambayo yangetokea kwa jamii endapo bangi hizo zingetumika, na mhukumu mshtakiwa adhabu ya kifungo cha maisha ili liwe fundisho kwake kuwa kujihusisha na jinai hakulipi.’’

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na mawakili wa Serikali wawili ambao ni Mess Mafuru na Jumanne Milanzi na upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili Bahati Hacks na inadaiwa kuwa mshtakiwa alikamatwa Februari 8, 2022 nyumbani kwake katika kijiji cha Kitonga Wilaya Mvomero mkoani Morogoro akiwa bangi hizo zilizokuwa zimefungwa kwenye viroba kumi.

Mafuriko yauwa 109 mikoa ya Magharibi, Kaskazini
Sadio Mane kurudishwa Ligi Kuu ya England