Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Singida, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa mtaa wa Kimpungua, manispaa ya Singida, Hamisi Mtanda (37), kwa kosa la ubakaji.

Mtanda, amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike, mwenye umri wa miaka 11.

Mwanasheria wa Serikali, Elizabeth Barabara, amesema mshtakiwa alianza kufanya mapenzi na mtoto wake huyo (jina linahifadhiwa) kuanzia Julai, mwaka jana (2019), kwa kumchokonoa kwa vidole baada ya kutengana na mama wa mtoto huyo.

Barabara amedai kuwa katika kipindi chote hicho, mshtakiwa huyo kabla ya kuanza kumwingilia kimwili mtoto ambaye ni mwanafunzi alikuwa akimnyemelea usiku akiwa amelala.

Amesema, mshtakiwa baada ya kuona sehemu za siri za mtoto zimetanuka, ndipo alipoanza kumwingilia kimwili na wakati akifanya unyama huo, mtoto alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata.

Kabla ya kutolewa adhabu, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea na kudai kuwa hakufanya unyama huo bali mtoto huyo alikuwa amefanya vitendo vya ngono na mwalimu, bila kumtaja ni mwalimu yupi.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi Robert Oguda, amesema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 30 jela, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama za mshtakiwa huyo.

AU yaikomalia Mali
Serikali kuzalisha korosho tani milioni moja

Comments

comments