Mchambuzi Nguli wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari amemvaa Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara kwa mara nyingine, kufutia andiko lake la kukebehi mchezo wa Kirafiki wa Simba SC dhidi ya Ismailia ya Misri.

Simba SC ilicheza mchezo wa kwanza wa Kirafiki jana Jumapili (Julai 17), ikiwa kambini nchini Misri ilikoweka Kambi ya Maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23 na kuambulia sare ya 1-1.

Manara aliikebehi taarifa ya mchezo huo, kwa madai Simba SC ilidanganya, kwani Ismailia ilicheza mchezo wa Ligi ya Misri siku ya Jumamosi (Julai 16) ugenini, hivyo ilikua ni vigumu kwa timu hiyo kucheza tena Jumapili.

Jemedari amemjibu Manara kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kwa kuweka Video ya Msemaji huyo wa Young Africans, alipokuwa Simba akisema Simba ina Kikosi kipana na inaweza Kucheza Mechi zaidi ya 3 kwa wakati Mmoja, Kisha Kuandika Ujumbe huu: “Tumewekeza kwenye UJINGA UJINGA na kwa kuwa mashabiki wetu ni WEPESI WEPESI basi ni rahisi tu kuwapeperusha, sasa kama mtu hana uwezo wa kuhoji mambo madogo madogo ya nini uhangaike nae, unampeperusha tu.”

Ukisogeza video utamuona mtu huyu anaeongea hapo kwamba Simba inaweza kucheza mechi 2 kwa siku 1, akikataa kwamba Ismaily haiwezi kucheza mechi 2 kwa siku 2 tofauti.

NB: Ogopa sana watu wanaoweza kuuza utu wao kwa vipande vya pesa. Watu hao Mwalimu Nyerere aliwaita mercenaries

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)

Haji Manara aliweka ujumbe katika Ukurasa wake wa Instagram akidai Simba SC haikucheza dhidi ya Ismailia na badala yake ilicheza na Madereva Taxi wa mji wa Ismailia.

Manara aliandika: Ismailia Wamecheza Jana mechi ya ligi ya kwao, leo mnawapiga fix mazuzu wenu,,Eti mmecheza nao mechi.

Nyieeee,,Yaan Jana wacheze mechi ya ligi tena away,,kisha leo mcheze nao mechi ya kirafiki?
Kuweni Serious,,Waambieni ukweli Wafuasi wenu,, Leo mmecheza na Madreva Taxi wanaoshabikia hyo Club,,na Parking za Taxi zao ni nje ya Uwanja wa Ismailia,,kuvaa jezi za Ismailia sio kigezo,,kwani mkisema ukweli mtakufa?

Nb:: Makolo 1- Ismailia Taxi Drivers 1

Period
Byuti Byuti

Ni Homa ya Mgunda mlipuko wa ugonjwa Lindi
Kagera mbioni kupata umeme wa gridi ya Taifa