Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeshauriwa kukaa chini na Wachezaji Shomari Salum Kapombe na Israel Patrick Mwenda, ili kumaliza tofauti zinazotajwa kuwepo baina yao.
Inaelezwa kuwa Wawili hao hawapiki chungu kimoja kwa matatizo yao binafsi, hali ambayo imepelekea kila mmoja kumkataa mwenzake wanapokuwa kambini.
Ushauri huo kwa Viongozi wa Simba SC umetolewa na Mdau wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari, alipozungumza katika kipindi cha Sports HQ cha EFM Radio leo Ijumaa (Januari 13), baada ya kuibuka kwa taarifa za Israel Patrick kuachwa kwenye safari ya Falme za Kiarabu.
“Kapombe na Mwenda wote ni vijana wangu niliwaona wakianza kucheza.Kapombe ana uwezo mkubwa kumzidi Mwenda.Ana uzoefu,lakini bwana mdogo Mwenda nae ni mahiri kiwanjani.Anapiga faulo.”
“Lakini kubwa viongozi wa Simba wanatakiwa kujua jinsi ya kuishi na wachezaji wao,maana ndani yake kuna mambo ya Misumari, binafsi kama mchezaji nimewahi kupigwa Misumari na nimewahi kupiga Misumari pia”
“Tunategemea Shomari atamuacha Mwenda kiwanjani, ina maana Shomari akiondoka Simba watatafuta mtu mwingine?” amehoji Jemedari Said