Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Abdulrahaman Kinana amewashauri na kuwakumbusha wanasiasa wa upinzani, kuheshimu fursa ya maridhiano ya kisiasa iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kinana ameyasema hayo mjini Tabora, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Mara, Simiyu na Tabora kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 na uhai wa Chama.

Amesema, “Niwasihi ndugu hatukatai mtoe hoja, hatukatai mseme yale mnayotaka kusema lakini semeni kwa uungwana, zungumzeni kwa busara, jengeni hoja, kumsema wewe sema mkataba huu haujakaa  vizuri, utaeleweka, toa hoja kwa nini hauajakaa vizuri.”

Aidha, Kinana pia alitumia fursa hiyo kuelezea mchakato wa kupata maridhiano ambayo yametoa fursa ya wananchi wakiwamo wanasiasa kuwa na uhuru wa kutoa maoni.

Hatuna tatizo na EWURA - TAOMAC
Juhudi utafutaji waliozama Ziwa Victoria zaendelea