Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wakulima kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba ya Chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, ili kuendana na hali ya hewa ya Tanzania.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo Agosti 8, 2023 wakati akifunga rasmi maonesho ya wakulima Nane – Nane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.”
Amesema, “nawapongeza mamilioni ya Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kwa juhudi zenu katika uzalishaji, Kazi zenu za kila siku zinaipa nchi yetu si tu uhakika wa chakula lakini pia ajira (zaidi ya asilimia 65), malighafi kwa viwanda vyetu (zaidi ya asilimia 60), na zinachangia zaidi ya robo ya Pato la Taifa letu.”
Aidha, Dkt. Samia pia ameongeza kuwa, “Serikali itaendelea kutoa ruzuku katika mbolea na pembejeo. Nimeagiza Wizara ya Kilimo kukaa na Wizara ya Fedha ili kuondoa gharama za kusambaza mbolea kwa ngazi ya kata ambazo zinafanya bei ya mboleo kwa mkulima kuwa juu.”