Kiungo kutoka nchini Uholanzi Jeremain Lens, amekamilisha taratibu za kujiunga klabu ya Sunderland ya nchini Uingereza akitokea Urusi kwenye klabu ya Dynamo Kiev.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amekamilisha mpango huo sanjari na kusaini mkataba wa miaka minne ambao utamuwezesha kuwatumikia paka weusi mpaka mwaka 2019.

Lens, aliwahi kufanya kazi na meneja wa sasa wa klabu ya Sunderland, Dick wakati akiitumikia klabu za PSV Eindhoven pamoja na AZ Alkmaar, zote za nchini Uholanzi na ukaribu wa wawili hao unatajwa kufanikisha mpango wa kukutana tena nchini Uingereza.

Ada ya usajili wa kiungo huyo inatajwa kuwa ni paund million 8 sawa na dola za kimarekani 12.51.

Liverpool Yatangaza Jezi ya Robert de Oliveira Na Kikosi Chake
Diamond na Vanessa watajwa tuzo za ‘Entertainment Africa’ za Marekani